Biblia Todo Logo
Bìoball air-loidhne

- Sanasan -

Zaburi 122 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002


Sifa za Yerusalema

1 Wimbo wa Safari za kidini. Wa Daudi. Nilifurahi waliponiambia: “Twende kwenye nyumba ya Yawe.”

2 Sasa tuko tumesimama kwenye milango yako, ee Yerusalema!

3 Yerusalema ni muji uliojengwa kusudi makundi ya watu yakutane humo.

4 Humo ndimo makabila yanamofika, ndiyo, makabila ya Yawe, kwa kumushukuru Yawe kama Waisraeli walivyoagiza.

5 Humo kulikuwa viti vya kifalme kwa kuamua maneno, ndivyo viti vya ukoo wa Daudi.

6 Muuombee Yerusalema amani mukisema: “Wote wanaokupenda wakae katika amani!

7 Ndani ya kuta zinazokuzunguka kuwe amani, nao usalama ukuwe ndani ya nyumba zako nzuri!”

8 Kwa ajili ya jamaa na wandugu zangu, ee Yerusalema, ninakutakia amani!

9 Kwa ajili ya nyumba ya Yawe, Mungu wetu, ninakuombea upate uheri!

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
Lean sinn:



Sanasan