Biblia Todo Logo
Bìoball air-loidhne

- Sanasan -

Zaburi 121 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002


Mungu ni mulinzi wetu

1 Wimbo wa safari za kidini. Ninainua macho kwenye milima. Musaada wangu unatoka wapi?

2 Musaada wangu unatoka kwa Yawe, aliyeumba mbingu na dunia.

3 Hatakuacha uanguke; mulinzi wako hasinzii.

4 Kweli mulinzi wa Israeli hasinzii wala halali.

5 Yawe ni mulinzi wako; yuko upande wako wa kuume kwa kukukinga.

6 Muchana jua halitakuchoma, wala mwezi hautakuzuru usiku.

7 Yawe atakukinga na uovu wote; atayalinda salama maisha yako.

8 Yawe atakulinda katika shuguli zako zote tangu sasa na hata milele.

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
Lean sinn:



Sanasan