Zaburi 111 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002Mungu anasifiwa kwa matendo yake 1 Haleluia! Nitamushukuru Yawe kwa moyo wangu wote, katika mukutano wa watu wa usawa. 2 Matendo ya Yawe ni makubwa sana! Wote wanaoyafurahia wanayachunguza. 3 Kila anachofanya kimejaa utukufu na heshima; haki yake inadumu milele. 4 Amesababisha matendo yake ya ajabu yakumbukwe; Yawe ni mwenye huruma na rehema. 5 Anawapa chakula wenye kumwabudu; hasahau hata kidogo agano lake. 6 Amewaonyesha watu wake nguvu ya matendo yake, amewapa inchi za mataifa mengine zikuwe mali yao. 7 Matendo yake ni ya haki na ya kuaminika; kanuni zake zote ni za kutegemewa siku zote. 8 Amri zake zinadumu milele; zimetolewa kwa uaminifu na usawa. 9 Aliwakomboa watu wake na kufanya nao agano la milele. Yeye ni mutakatifu na wa kutisha sana! 10 Kumwogopa Yawe ni musingi wa hekima; wote wanaotii amri zake wanajaliwa akili. Sifa zake zinadumu milele. |
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.
Bible Society of the Democratic Republic of Congo