Zaburi 110 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002Kusimikwa kwa mufalme muchaguliwa 1 Zaburi ya Daudi. Yawe anamwambia bwana wangu: “Ikaa na mamlaka kwa kuume kwangu mpaka nitakapowaweka waadui zako chini ya miguu yako.” 2 Yawe ataeneza mamlaka yako kutoka Sayuni; utatawala juu ya waadui zako wote. 3 Watu wako watajitolea, siku utakapokwenda kuwapiga waadui. Juu ya milima mitakatifu vijana wako watakufikia, kama umande unaotokeza asubui mapema. 4 Yawe amekuapia hivi wala hatabadilisha nia yake: “Wewe ni kuhani milele kwa utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.” 5 Bwana wetu yuko karibu nawe; atawaponda wafalme atakapokasirika. 6 Atayahukumu mataifa na kuwaua watu wengi; atawaponda waongozi kila nafasi katika dunia. 7 Mufalme atakunywa maji ya kijito katika njia, kisha atainua kichwa kwa ushindi. |
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.
Bible Society of the Democratic Republic of Congo