Biblia Todo Logo
Bìoball air-loidhne

- Sanasan -

Zaburi 108 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002


Maombi ya kujikinga na waadui
( Zab 57.7-11 ; 60.5-12 )

1 Zaburi ya Daudi: Wimbo.

2 Moyo wangu ni tayari, ee Mungu. Moyo wangu ni tayari. Nitaimba na kukushangilia! Amuka, ee nafsi yangu!

3 Muamuke, enyi kinubi na zeze! Nitaamusha mapambazuko!

4 Ee Yawe, nitakushukuru kati ya mataifa; nitakuimbia sifa kati ya mataifa.

5 Wema wako ni mukubwa kuliko mbingu; uaminifu wako unaenea hata kwenye mawingu.

6 Utukuzwe, ee Mungu, juu ya mbingu! Utukufu wako uenee katika dunia yote!

7 Ukomboe watu hao unaowapenda; utusaidie kwa mukono wako na kutusikiliza.

8 Mungu amesema toka hekalu lake takatifu: “Sasa nitakwenda kwa shangwe kugawanya Sekemu, bonde la Sukoti nitalipima sehemu sehemu.

9 Gileadi ni yangu na Manase ni yangu; Efuraimu ni kofia yangu ya chuma, na Yuda ni fimbo yangu ya kifalme.

10 Moabu ni kama bakuli langu la kunawia; nitatupia kiatu changu katika Edomu kwa kuirizi, nitapiga kelele la ushindi juu ya Wafilistini!”

11 Ni nani atakayenipeleka katika muji unaozungukwa na kuta? Ni nani atakayeniongoza mpaka Edomu?

12 Ee Mungu, umetuacha kabisa? Wewe hauendi tena na makundi yetu ya waaskari!

13 Utupatie musaada juu ya waadui zetu, maana musaada wa mwanadamu haufai kitu.

14 Mungu akikuwa upande wetu, tutashinda. Yeye ndiye atakayewaponda waadui zetu.

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
Lean sinn:



Sanasan