Yona 2 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 20021 Kisha, Yawe akaamuru samaki mukubwa amumeze Yona, naye akabaki ndani ya tumbo la samaki huyo kwa muda wa siku tatu, usiku na muchana. Maombi ya Yona 2 Basi, Yona akiwa ndani ya tumbo la samaki yule, akamwomba Yawe Mungu wake, 3 akisema: Kwa sababu ya taabu yangu, nilikuomba, ee Yawe, nawe ukanisikiliza; toka chini kuzimu, nilikulilia, nawe ukasikiliza kilio changu. 4 Ulinitupa katika kilindi, katikati ya bahari, maji mengi yakanizunguka, mawimbi na maji mengi vikapita juu yangu. 5 Nilizani kwamba nimetupwa mbali nawe; nisiweze kuliona tena hekalu lako takatifu. 6 Maji yalinizunguka na kunisonga; kilindi kilinifikia kila upande, majani ya bahari yakanifunika kichwa. 7 Niliteremuka mpaka kwenye misingi ya milima, katika inchi ambayo milango yake imefungwa milele. Lakini wewe, ee Yawe, Mungu wangu, umenipandisha nikiwa muzima kutoka mule ndani ya shimo. 8 Roho yangu ilipoanza kunitoka, nilikukumbuka, ee Yawe, maombi yangu yakakufikia katika hekalu lako takatifu. 9 Watu wanaoabudu sanamu za miungu ya bure, wanautupilia mbali uaminifu wao kwako. 10 Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani, nitakutolea sadaka, na kutimiza viapo vyangu. Yawe, ndiye anayeokoa. 11 Basi, Yawe akamwamuru yule samaki, naye akamutapika Yona kwenye inchi kavu. |
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.
Bible Society of the Democratic Republic of Congo