Biblia Todo Logo
Bìoball air-loidhne

- Sanasan -

Yobu 16 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

1 Halafu Yobu akajibu:

2 Mambo kama yale nimeyasikia mengi; ninyi ni wafariji wenye kutaabisha!

3 Mwisho wa maneno haya ya bure ni wakati gani? Au ni kitu gani kinachowasukuma kujibu?

4 Kama mungekuwa mimi, na mimi ninyi, ningeweza kusema kama ninyi. Ningeweza kutunga maneno juu yenu, na kutikisa kichwa changu.

5 Ningeweza kuwatia moyo kwa maneno yangu, na maneno yangu ya faraja yangewatuliza.

6 Lakini nikisema maumivu yangu hayatulii, na nikikaa kimya hayaondoki.

7 Kweli Mungu amenichakalisha, ameharibu kila kitu karibu nami.

8 Amenifanya ninyauke na huo ni ushuhuda juu yangu. Kukonda kwangu kumenishitaki na kushuhudia juu yangu.

9 Amenirarua kwa hasira na kunichukia, amenisagia meno, na adui yangu ananitonolea macho.

10 Watu wanafungua vinywa vyao na kunichekelea. Makundi kwa makundi wananizunguka na kunipiga makofi kwenye mashavu.

11 Mungu amenitia katika mikono ya wapotovu na kunitupa katika mikono ya waovu.

12 Nilikuwa nimestarehe, lakini akanivunjavunja. Alinikamatia katika shingo na kunipasua vipandevipande. Akanifanya shabaha ya mishale yake,

13 akanipiga mishale kutoka kila upande. Amenipasua figo bila huruma, na nyongo yangu akaimwanga chini.

14 Ananivunja na kunipiga tena na tena; ananishambulia kama askari.

15 Nimejishonea nguo za gunia; utukufu wangu nikautupa katika mavumbi.

16 Macho yangu ni mekundu kwa sababu ya kulia, kope zangu zimekuwa nyeusi sana,

17 ingawa sijatesa watu kwa mukono wangu, na maombi yangu kwa Mungu ni safi.

18 Ewe dunia, usifunike damu yangu iliyomwangika; kilio changu kienee kila pahali.

19 Nina uhakika kwamba nina mushuhuda wangu mbinguni; mwenye kunitetea yuko kule juu.

20 Warafiki zangu wanizarau; ninatoa machozi kumwomba Mungu.

21 Heri mutu angenitetea mbele ya Mungu, kama vile inavyofanyika katika dunia kati ya watu wawili.

22 Kweli, miaka yangu ni michache, nami nitakwenda kule ambako sitarudi.

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
Lean sinn:



Sanasan