Yeremia 45 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002Ahadi ya Mungu kwa Baruku 1 Haya ndiyo maneno nabii Yeremia aliyosema katika mwaka wa ine wa utawala wa Yoyakimu mwana wa Yosia, mufalme wa Yuda na Baruku mwana wa Neria akayaandika katika kitabu: 2 Yawe, Mungu wa Israeli, anasema hivi juu yako wewe Baruku: 3 Wewe ulisema: Ole wangu! Yawe ameongezea uchungu juu ya maumivu yangu. Nimechoka na kulalamika, wala siwezi kupumzika. 4 Lakini Yawe ameniambia nikuambie: Yawe anasema hivi: Yale niliyojenga ninayabomoa, na yale niliyopanda ninayaongoa; nitafanya hivyo katika inchi yote. 5 Wewe unajitakia wewe mwenyewe mambo makubwamakubwa? Usiyatafute! Achana nayo, maana ninaleta maangamizi juu ya wanadamu wote. Pato lako ni hili: nitayaokoa maisha yako kila nafasi utakapokwenda. –Ni ujumbe wa Yawe. |
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.
Bible Society of the Democratic Republic of Congo