Biblia Todo Logo
Bìoball air-loidhne

- Sanasan -

Mwanzo 5 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002


Wazao wa Adamu
( 1 Sik 1.1-4 )

1 Hiki ndicho kitabu cha uzao wa Adamu. Wakati Mungu alipowaumba wanadamu, aliwaumba kwa mufano wake.

2 Aliwaumba mwanaume na mwanamuke, kisha akawabariki na kuwapa jina “Wanadamu” siku ileile alipowaumba.

3 Adamu alipokuwa na umri wa miaka mia moja na makumi tatu, alipata mutoto aliyefanana naye, na mwenye sura kama yake; akamwita Seti.

4 Kisha kuzaa Seti, Adamu akaishi miaka mia nane, na kupata wana wengine na wabinti.

5 Adamu alikufa akiwa na umri wa miaka mia tisa na makumi tatu.

6 Wakati Seti alipokuwa na umri wa miaka mia moja na mitano, akazaa Enosi.

7 Kisha kuzaa Enosi, Seti akaishi miaka mia nane na saba, na kupata wana wengine na wabinti.

8 Seti akakufa akiwa na umri wa miaka mia tisa kumi na miwili.

9 Wakati Enosi alipokuwa na umri wa miaka makumi tisa, akazaa Kenani.

10 Kisha kuzaa Kenani, Enosi akaishi miaka mia nane kumi na mitano, na kupata wana wengine na wabinti.

11 Enosi akakufa akiwa na umri wa miaka mia tisa na mitano.

12 Wakati Kenani alipokuwa na umri wa miaka makumi saba, akazaa Mahalaleli.

13 Kisha kuzaa Mahalaleli, Kenani akaishi miaka mia nane na makumi ine, na kupata wana wengine na wabinti.

14 Kenani alikufa akiwa na umri wa miaka mia tisa na kumi.

15 Wakati Mahalaleli alipokuwa na umri wa miaka makumi sita na mitano, akazaa Yaredi.

16 Kisha kuzaa Yaredi, Mahalaleli akaishi miaka mia nane na makumi tatu, na kupata wana wengine na wabinti.

17 Mahalaleli akakufa akiwa na umri wa miaka mia nane makumi tisa na mitano.

18 Wakati Yaredi alipokuwa na umri wa miaka mia moja makumi sita na miwili, akazaa Henoki.

19 Kisha kuzaa Henoki, Yaredi akaishi miaka mia nane, na kupata wana wengine na wabinti.

20 Yaredi akakufa akiwa na umri wa miaka mia tisa makumi sita na miwili.

21 Wakati Enoki alipokuwa na umri wa miaka makumi sita na mitano, akazaa Metusela.

22 Enoki alikuwa anashirikiana na Mungu. Kisha kuzaa Metusela, Enoki aliishi miaka mia tatu, na kupata wana wengine na wabinti.

23 Enoki aliishi miaka mia tatu makumi sita na mitano.

24 Alikuwa akishirikiana na Mungu, akatoweka, kwa maana Mungu alimupeleka.

25 Wakati Metusela alipokuwa na umri wa miaka mia moja makumi nane na saba, akazaa Lameki.

26 Kisha kuzaa Lameki, Metusela akaishi miaka mia saba makumi nane na miwili, na kupata wana wengine na wabinti.

27 Metusela akakufa akiwa na umri wa miaka mia tisa makumi sita na tisa.

28 Wakati Lameki alipokuwa na umri wa miaka mia moja makumi nane na miwili, akazaa mutoto mwanaume.

29 Akamwita mutoto yule Noa, akisema: “Mutoto huyu ndiye atakayetufariji kutokana na kazi yetu ngumu tunayofanya kwa mikono yetu katika inchi ambayo Yawe alilaani.”

30 Kisha kuzaa Noa, Lameki akaishi miaka mia tano makumi kenda na mitano, na kupata wana wengine na wabinti.

31 Lameki akakufa akiwa na umri wa miaka mia saba makumi saba na saba.

32 Kisha Noa kutimiza umri wa miaka mia tano, akazaa Semu na Hamu na Yafeti.

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
Lean sinn:



Sanasan