Biblia Todo Logo
Bìoball air-loidhne

- Sanasan -

Mwanzo 10 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002


Wazao wa Noa

1 Nyuma ya mafuriko ya maji, Semu, Hamu na Yafeti, wana wa Noa, walipata watoto wanaume na wanawake. Hawa ndio wazao wao:

2 Wana wa Yafeti walikuwa Gomeri, Magogi, Madayi, Yavani, Tubali, Meseki na Tirasi.

3 Wana wa Gomeri walikuwa Askenazi, Rifati na Togarma.

4 Wana wa Yavani walikuwa Elisa, Tarsisi, Kitimu na Rodanimu.

5 Kutokana na hawa visanga vya watu wa mataifa mengine vikagawanywa kwa inchi zao, kila watu kwa luga yao, kwa jamaa zao, kufuatana na mataifa yao.

6 Wana wa Hamu walikuwa Kushi, Misiraimu, Puti na Kanana.

7 Wana wa Kushi walikuwa Seba, Havila, Sabuta, Rama na Sabuteka. Wana wa Rama walikuwa Seba na Dedani.

8 Kushi alikuwa baba ya Nimurodi ambaye alikuwa shujaa wa kwanza katika dunia.

9 Alikuwa mwindaji shujaa mbele ya Yawe, ndiyo maana kuna musemo unaosema: “Kama vile Nimurodi mwindaji shujaa mbele ya Yawe.”

10 Miji ya kwanza ya utawala wake ilikuwa Babeli, Ereki, na Akadi katika inchi ya Sinari.

11 Kutoka kule, Nimurodi alikwenda Asuria, akajenga miji ya Ninawe, Rehoboti-Iri, Kala na

12 Reseni unaokuwa kati ya Ninawe na muji mukubwa wa Kala.

13 Misiraimu alikuwa babu ya Waludi, Waanamu, Walehabi, Wanafutuhi,

14 Wapatirusi, Wakasiluhi (ambao ndio shina ya Wafilistini), na Wakafutorimu.

15 Kanana alikuwa babu ya Sidona, muzaliwa wake wa kwanza, na Heti,

16 na vilevile babu ya Wayebusi, Waamori, Wagirgasi,

17 Wahivi, Waarki, Wasini,

18 Waarwadi, Wazemari na Wahamati. Na nyuma watu wa jamaa mbalimbali za Kanana wakatawanyika,

19 hata eneo la inchi yao likakuwa toka Sidona kuelekea upande wa kusini, kuendelea Gerari mpaka Gaza, na kuelekea upande wa mashariki liliendelea kwa Sodoma na Gomora, Adima na Seboimu mpaka Lasa.

20 Hao ndio wazao wa Hamu kufuatana na makabila yao, luga zao, inchi zao na mataifa yao.

21 Semu, mukubwa wa Yafeti, alikuwa baba ya Waebrania wote.

22 Wana wa Semu walikuwa Elamu, Asuri, Aripakisadi, Ludi na Aramu.

23 Wana wa Aramu walikuwa Usi, Huli, Geteri na Masi.

24 Aripakisadi alizaa Sela, Sela akazaa Eberi.

25 Eberi alikuwa na wana wawili: wa kwanza akamwita Pelegi kwa sababu wakati ule watu katika dunia waligawanyika na wa pili akamwita Yokitani.

26 Yokitani alikuwa baba ya Almodadi, Selefu, Hazarimaweti, Yera,

27 Hadoramu, Uzali, Dikela,

28 Obali, Abimaeli, Seba,

29 Ofiri, Havila na Yobabu. Hao wote walikuwa wana wa Yokitani.

30 Inchi walimokaa ilienea toka Mesa mpaka Sefari katika inchi ya vilima vya upande wa mashariki.

31 Hao ndio wazao wa Semu, kufuatana na makabila yao, luga zao, inchi zao na mataifa yao.

32 Hao ndio jamaa za wana wa Noa, kufuatana na vizazi vyao na mataifa yao. Kutokana nao, mataifa yote yalienea katika dunia nyuma ya mafuriko ya maji.

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
Lean sinn:



Sanasan