Biblia Todo Logo
Bìoball air-loidhne

- Sanasan -

Mezali 2 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002


Mafaa ya hekima

1 Mwana wangu, ukikubali maneno yangu, na kushika maagizo yangu,

2 ukitega sikio lako kwa kusikiliza hekima, na kuelekeza moyo wako upate ufahamu,

3 ukiomba upewe akili, ukisihi upewe ufahamu,

4 ukitafuta hekima kama feza, na kuitaka kama hazina iliyofichwa,

5 utaelewa maana ya kumwogopa Yawe, utafahamu maana ya kumujua Mungu.

6 Maana Yawe anawapa watu hekima; katika kinywa chake kunatoka maarifa na ufahamu.

7 Anawawekea watu wa usawa akiba ya hekima safi, yeye ni ngao kwa watu wanaoishi kwa ukamilifu.

8 Analinda mienendo ya watu wanaofuata sheria yake, na kuchunga njia za waaminifu wake.

9 Ukinisikiliza, utafahamu haki, usawa, na kufuata sheria ya Mungu; utafahamu kila njia nzuri.

10 Maana hekima itaingia ndani ya moyo wako, na maarifa yatapendeza nafsi yako.

11 Hekima itakulinda, ufahamu utakuchunga;

12 vitakuepusha na njia ya uovu, na watu wa maneno mapotovu,

13 watu wanaoacha njia zenye kunyooka kwa kufuata njia za giza,

14 watu wanaofurahia kutenda maovu na kupendezwa na upotovu wa maovu,

15 watu ambao mienendo yao imepotoka, nazo njia zao haziaminiki.

16 Utaepukana na mwanamuke mwasherati, mwanamuke kahaba wa maneno matamu,

17 mwanamuke anayemwacha mwenzake wa ujana wake, na kusahau agano la Mungu wake.

18 Nyumba yake inaelekea kifo, njia zake zinakwenda kuzimu.

19 Yeyote anayemwendea harudi hata kidogo, wala harudilii tena njia ya uzima.

20 Kwa hiyo utafuata mufano wa watu wazuri, na kufuata mienendo ya wenye haki.

21 Maana watu wa usawa watarizi inchi, na watu wakamilifu watadumu ndani yake.

22 Lakini waovu wataondolewa katika inchi, na watu wabaya watangolewa toka ndani yake.

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
Lean sinn:



Sanasan