Biblia Todo Logo
Bìoball air-loidhne

- Sanasan -

Marko 16 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002


Ufufuko wa Yesu
( Mat 28.1-8 ; Lk 24.1-12 ; Yn 20.1-10 )

1 Siku ya Sabato ilipokwisha kupita, Maria wa Magdala, na Maria mama ya Yakobo, na mwanamuke mwingine Salome, walinunua marasi kusudi waende kupakaa maiti ya Yesu.

2 Siku ya kwanza ya juma, asubui mapema, wakati jua lilipoanza kutokea, wakaenda kwenye kaburi.

3 Nao walienda wakiulizana: “Ni nani atakayetusukumia lile jiwe kutoka kwenye kiingilio cha kaburi?”

4 Lakini walipoinua macho, wakaona kwamba lile jiwe lilikuwa limekwisha kusukumwa pembeni. (Jiwe lile lilikuwa kubwa sana.)

5 Basi wakaingia ndani ya kaburi, na mule wakaona kijana mumoja akiikaa upande wa kuume, akivaa kanzu nyeupe. Nao wakashituka.

6 Lakini kijana yule akawaambia: “Musishituke! Munamutafuta Yesu wa Nazareti aliyetundikwa juu ya musalaba. Yeye amefufuka, hayuko hapa. Muangalie, hapa ni pahali walipomuweka.

7 Muende sasa kupasha habari kwa wanafunzi wake na kwa Petro, muwaambie kwamba anawatangulia Galilaya; nao watamwona kule sawa vile alivyowaambia.”

8 Basi walitoka kwenye kaburi na kukimbia mbio. Walikuwa wakitetemeka na kushangaa sana. Nao hawakumwambia mutu yeyote, kwa sababu waliogopa. [


Yesu anamutokea Maria wa Magdala
( Mat 28.9-10 ; Yn 20.11-18 )

9 Yesu alipokwisha kufufuka asubui mapema, siku ya kwanza ya juma, alimutokea kwanza Maria wa Magdala, yule aliyefukuza pepo saba toka ndani yake.

10 Huyu akaenda kupasha habari kwa wale waliokuwa wakikaa pamoja na Yesu. Walikuwa wakiomboleza na kulia.

11 Na waliposikia jinsi Maria alivyowaambia kwamba Yesu ni muzima, na kwamba amemwona, hawakumusadikia.


Yesu anawatokea wanafunzi wawili
( Lk 24.13-35 )

12 Kisha, Yesu akawatokea wanafunzi wawili, akiwa na sura ingine. Wanafunzi hao walikuwa wanakwenda kwenye vijiji.

13 Nao wakarudi na kuwapasha wanafunzi wengine habari ile, lakini wao vilevile hawakusadikia.


Yesu anawatokea wanafunzi kumi na mumoja
( Mat 28.16-20 ; Lk 24.36-49 ; Yn 20.19-23 ; Mdo 1.6-8 )

14 Kwa mwisho Yesu akawatokea wanafunzi kumi na mumoja walipokuwa wakikula. Naye akawakaripia kwa sababu ya kutokuamini kwao na kwa sababu ya ugumu wao. Kwa maana hawakusadikia wale waliomwona nyuma ya kufufuka kwake.

15 Kisha akawaambia: “Mwende katika dunia yote na kuhubiri Habari Njema kwa kila mutu.

16 Anayeamini na kubatizwa ataokolewa, lakini asiyeamini atahukumiwa.

17 Nao wote watakaoniamini watafanya vitambulisho hivi: watafukuza pepo kwa jina langu; watasema kwa luga mupya;

18 wakishika nyoka au kunywa sumu yoyote, hawatakufa. Wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapona.”


Yesu ananyanyuli mbinguni
(Mat 24.50-53; Mdo 1.9-11 )

19 Bwana Yesu alipokwisha kusema nao maneno hayo, akanyanyuliwa juu kwenda mbinguni na kuikaa kwa upande wa kuume wa Mungu.

20 Nao wanafunzi wakaenda kuhubiri fasi zote. Bwana akatumika pamoja nao na kuhakikisha ukweli wa mahubiri yao kwa njia ya vitambulisho walivyofanya.]

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
Lean sinn:



Sanasan