Biblia Todo Logo
Bìoball air-loidhne

- Sanasan -

Isaya 64 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

1 Ingeteketea kama moto unavyochoma kichaka, kama vile moto unavyochemusha maji. Ukuje upate kuwajulisha waadui zako jina lako nayo mataifa yatetemeke mbele yako!

2 Wakati ulipotenda maajabu ambayo hatukutazamia, ulishuka chini nayo milima ikatetemeka ilipokuona.

3 Tangu zamani hakuna aliyepata kusikia kwa masikio yake wala kumwona Mungu anayekuwa kama wewe, anayetenda mambo kama hayo kwa ajili ya wale wanaomutegemea!

4 Wewe unakuja kuwasaidia wanaotenda haki kwa furaha, wanaokukumbuka na kufuata njia zako. Ulitukasirikia tulipokuwa wenye zambi; sisi tumeasi kwa muda murefu.

5 Sisi wote tumekuwa kama watu wachafu; matendo yetu yote mema ni kama nguo chafu. Wote tunanyauka kama majani, uovu wetu unatupeperusha kama upepo.

6 Hakuna hata mumoja anayekuja kukuomba; hakuna anayejishugulisha kukutafuta. Wewe unauficha uso wako mbali nasi, umetuacha tufungwe na maovu yetu.

7 Hata hivyo, ee Yawe, wewe ni Baba yetu. Sisi ni kama udongo, wewe ni mufinyanzi. Sisi wote ni kazi ya mikono yako.

8 Usitukasirikie sana, ee Yawe, usiukumbuke uovu wetu siku zote! Ukumbuke kwamba sisi wote ni watu wako!

9 Miji yako mitakatifu imekuwa jangwa; Sayuni umekuwa matongo, Yerusalema umekuwa uharibifu.

10 Nyumba yetu takatifu na nzuri, ambamo babu zetu walikusifu, imeteketezwa kwa moto. Pahali petu pote pazuri pamekuwa mabomoko.

11 Mbele ya hayo yote utajizuiza usifanye kitu? Utaendelea kunyamaza tu, ee Yawe, na kututesa kupita kipimo?

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
Lean sinn:



Sanasan