Biblia Todo Logo
Bìoball air-loidhne

- Sanasan -

Isaya 61 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002


Habari njema ya wokovu

1 Roho wa Bwana wetu Yawe yuko pamoja nami, maana Yawe amenichagua, akanituma niwahubirie wanaoteswa habari njema, niwatunze waliovunjika moyo, niwatangazie waliohamishwa kwamba watapata uhuru, na wafungwa kwamba watafunguliwa.

2 Amenituma kutangaza mwaka wake wa neema, na siku ya Mungu wetu ya kulipiza kisasi kusudi niwafariji wote wanaoomboleza.

3 na kuwapa wale wanaoomboleza katika Sayuni taji la maua pahali pa majivu juu ya kichwa, mafuta ya kuangarisha kwa furaha pahali pa maombolezo, nguo ya sifa pahali pa moyo muzito. Nao wataitwa miti ya mialo ya haki, Yawe aliyopanda kuonyesha utukufu wake.

4 Watayajenga upya mabomoko ya zamani, wataisimika miji iliyoharibika tangu mbele; wataitengeneza miji iliyobomolewa, uharibifu wa vizazi vingi vilivyopita.

5 Wageni watakuwa hapo kuwachungia makundi yenu ya nyama; watawalimia na kuwatunzia mizabibu yenu.

6 Nanyi mutaitwa: “Makuhani wa Yawe”, Mutaitwa: “Watumishi wa Mungu wetu”. Mutafaidika kwa utajiri wa mataifa, mutatukuzwa kwa mali zao.

7 Kwa vile mulipata haya mara mbili, watu wakaona kwamba mazarau ni majaliwa yenu, sasa mutapata sehemu mara mbili kuwa mali yenu, na furaha yenu itadumu milele.

8 Mimi Yawe ninapenda watu wafuate sheria yangu; ninachukia unyanganyi na uovu. Nitawatunza watu wangu kwa uaminifu, nitafanya nao agano la milele.

9 Wazao wao watajulikana kati ya mataifa; watajulikana kati ya watu wengine. Kila mutu atakayewaona atakubali kwamba wao ni watu waliobarikiwa na Yawe.

10 Nitafurahi sana kwa sababu ya Yawe, nafsi yangu itashangilia kwa sababu ya Mungu wangu. Maana amenivalisha nguo ya wokovu, amenifunika kanzu ya haki, kama bwana arusi anavyojipamba kwa shada la maua, kama bibi arusi anavyojipamba kwa ushanga wake.

11 Hivyo, kama vile udongo unavyootesha mimea, na shamba linavyochipukiza mbegu zilizopandwa humo, Yawe atasababisha haki na sifa kuonekana mbele ya mataifa yote.

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
Lean sinn:



Sanasan