Biblia Todo Logo
Bìoball air-loidhne

- Sanasan -

Isaya 47 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002


Hukumu juu ya inchi ya Babeli

1 Shuka, uikae katika mavumbi, ewe bikira, binti wa Babeli! Ikaa chini pasipo kiti cha kifalme, ewe binti wa Wakaldea! Tokea sasa hautaitwa tena murembo wala mwenye kupendeza.

2 Utwae mawe ya kusagia, usage unga kama mutumwa! Vua kitambaa chako, pandisha kanzu yako! Onyesha miguu yako kwa kuvuka mito.

3 Watu watauona uchi wako; wataona haya yako. Mimi nitalipiza kisasi, wala sitamuhurumia mutu yeyote.

4 Mukombozi wetu ndiye Mutakatifu wa Israeli; Yawe wa majeshi ndilo jina lake.

5 Ikaa kimya, ingia katika giza, ewe taifa la Wakaldea. Maana umepoteza cheo yako ya kuwa malkia wa falme.

6 Niliwakasirikia watu wangu, Israeli, nikawafanya watu wangu kuwa wanaharamu. Niliwatia katika mikono yako, nawe haukuwaonea huruma; na wazee uliwabebesha nira nzito sana.

7 Ulijisemesha ndani ya moyo: “Nitakuwa malkia milele”, nawe haukufikiri juu ya mambo yanayotokea, wala kuwaza juu ya mwisho wake.

8 Sasa, basi, sikiliza, ewe mupenda raha, wewe unayezani kuwa katika usalama, na kujisemesha: Mimi ndiye. Hakuna mwingine isipokuwa mimi. Sitakuwa mujane hata kidogo, wala sitakufiwa na watoto wangu.

9 Haya yote mawili yatakupata kwa rafla katika siku moja: kupoteza watoto wako na kuwa mujane, ijapokuwa una wingi wa uchawi wako, na nguvu nyingi za uganga wako.

10 Ulijiona salama katika uovu wako; ukajisemesha: Hakuna mutu anayeniona. Hekima na elimu yako vilikupotosha, ukajisemesha ndani ya moyo wako: Mimi ndiye; hakuna mwingine isipokuwa mimi.

11 Lakini hasara itakupata ambayo hautaweza kujiepusha nayo. Magumu yatakutokea ambayo hautaweza kuyapinga; maangamizi yatakufikia kwa rafla ambayo haujapata kuyaona hata kidogo.

12 Endelea basi na uganga wako, tegemea wingi wa uchawi wako. Wewe uliyashugulikia tangu ujana wako ukitumainia kwamba utafanikiwa au kusababisha woga kwa watu!

13 Wewe umejichokesha bure na washauri wako. Basi, wajitokeze hao wenye akili wakuokoe! Wao wanagawanya mbingu sehemusehemu, wanachunguza nyota na kutabiri kila mwezi yatakayokupata.

14 Wao ni kama majani yenye kukauka: moto utayateketeza! Hawawezi hata kujiokoa wenyewe mbali na ukali wa moto huo. Moto huo si wa kujipatia joto, huo si moto wa kuota!

15 Ndivyo watakavyokuwa hao uliowategemea hivyo, hao uliojishugulisha nao tangu ujana wako. Watatangatanga kila mumoja njia yake; hakuna hata mumoja atakayeweza kukuokoa.

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
Lean sinn:



Sanasan