Biblia Todo Logo
Bìoball air-loidhne

- Sanasan -

Isaya 35 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

1 Mbuga na inchi kavu vitachangamuka, jangwa litafurahi na kuchanua maua.

2 Litachanua maua kwa wingi kama waridi, litashangilia na kuimba kwa furaha. Mungu atalijalia utukufu wa milima ya Lebanoni, uzuri wa mulima Karmeli na wa bonde la Saroni. Watu watauona utukufu wa Yawe, watauona ukubwa wa Mungu wetu.

3 Muimarishe mikono zaifu, mukaze magoti yanayoregea.

4 Muwaambie waliovunjika moyo: Mujipe moyo, musiogope! Muangalie Mungu wenu atakuja kulipiza kisasi, atakuja kuwaazibu waadui zenu; atakuja yeye mwenyewe kuwaokoa ninyi.

5 Hapo vipofu wataona tena, na viziwi watasikia tena.

6 Viwete watarukaruka kama paa, na bubu wataimba kwa furaha. Maji yatabubujika katika jangwa na vijito katika mbuga.

7 Muchanga wa moto katika jangwa utakuwa ziwa la maji, inchi kavu itabubujika vijito. Makao ya imbwa wa pori yatajaa maji; nyasi zitaota na kukomaa kama mianzi.

8 Humo kutakuwa barabara kubwa, nayo itaitwa Njia Takatifu. Watu wachafu hawatapitia humo, lakini wale watu wa Mungu tu; wapumbafu hawatakanyaga ndani yake,

9 humo hamutakuwa simba, nyama yeyote mukali hatapitia humo, hao hawatapatikana humo. Lakini waliokombolewa ndio watakaopita humo.

10 Waliokombolewa na Yawe watarudi, watakuja Sayuni wakipiga vigelegele. Watakuwa wenye furaha ya milele, watajaliwa furaha na shangwe; huzuni na kilio vitatoweka kabisa.

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
Lean sinn:



Sanasan