Biblia Todo Logo
Bìoball air-loidhne

- Sanasan -

Isaya 25 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002


Wimbo wa sifa kwa Mungu

1 Wewe, ee Yawe, ndiwe Mungu wangu; nitakutukuza na kulisifu jina lako, kwa maana umetenda mambo ya ajabu; unaitimiza kwa uaminifu na kweli mipango uliyoipanga tangu zamani.

2 Umeufanya muji kuwa lundo la mawe, muji wenye pango kuwa uharibifu. Nyumba za watu wageni zimetoweka, wala hazitajengwa tena upya.

3 Kwa hiyo watu wenye nguvu watakutukuza, miji ya mataifa kali itakuogopa.

4 Maana wewe umekuwa kimbilio kwa wazaifu, pango kwa wakosefu katika taabu zao. Wewe ni kimbilio wakati wa zoruba, kivuli wakati wa joto kali. Kweli pigo la watu wakali ni kali kama zoruba inayopiga ukuta;

5 ni kama joto la jua juu ya inchi kavu. Lakini wewe unakomesha fujo ya wageni. Kama wingu linavyofifisha joto la jua, ndivyo unavyokomesha nyimbo za ushindi za watu wakali.

6 Juu ya mulima Sayuni, Yawe wa majeshi atawafanyia watu wote karamu ya nyama zenye kunona na divai nzuri, nyama tamu zenye mafuta, pamoja na divai safi.

7 Katika mulima huuhuu, Yawe ataliondoa wingu la huzuni lililowafunika watu wote, kifuniko cha uchungu juu ya mataifa yote.

8 Bwana wetu Yawe atakiangamiza kifo milele! Atayafuta machozi katika nyuso za watu wote na kuondoa haya ya watu wake katika dunia yote. Yawe amesema hivyo.

9 Siku ile, watu wote watasema: Huyu ndiye Mungu wetu! Tumemungojea atuokoe. Huyu ndiye Yawe tuliyemutazamia. Mukuje tufurahi na kushangilia kwa sababu ametuokoa.


Mungu ataiazibu Moabu

10 Yawe ataulinda mulima wa Sayuni, lakini watu wa Moabu watakanyagwakanyagwa ndani ya inchi yao kama nyasi katika shimo la mboleo.

11 Watainyoosha mikono yao kama mutu anayejaribu kuogelea, lakini pamoja na bidii yao, Yawe ataporomosha kiburi chao.

12 Atabomoa pango za miji ya Moabu yenye kuta ndefu na kuiangusha chini ndani ya mavumbi.

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
Lean sinn:



Sanasan