Biblia Todo Logo
Bìoball air-loidhne

- Sanasan -

1 Mambo ya Siku 8 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002


Wazao wa Benjamina

1 Benjamina alizaa wana hawa: Bela, muzaliwa wake wa kwanza; Asibeli, wa pili; Ahara, wa tatu;

2 Noha, wa ine; na Rafa, wa tano.

3 Wana wa Bela walikuwa: Adari, Gera, Abihudi,

4 Abisua, Namani, Ahoa,

5 Gera, Sefufanu na Huramu.

6 Hawa ndio wazao wa Ehudu waliokuwa viongozi wa jamaa za wale waliokuwa wakiishi Geba, lakini wakapelekwa katika uhamisho kule Manahati:

7 Namani, Ahiya na Gera. Gera, baba ya Uza na Ahihudi, ndiye aliyewaongoza walipohamishwa.

8 Saharaimu alizaa watoto katika inchi ya Moabu, nyuma ya kufukuza wanawake wake Husimu na Bara.

9 Kisha aliishi katika inchi ya Moabu, akamwoa Hodesi, naye akamuzalia wana hawa: Yoabu, Sibia, Mesa, Malakamu,

10 Yeusi, Sakia, na Mirma. Hawa wana wake wote walikuja kuwa wakubwa wa ukoo.

11 Husimu muke wa Saharaimu alimuzaliwa wana wengine wawili: Abitubu na Elipali.

12 Wana wa Elipali walikuwa: Eberi, Misamu na Semedi ambaye alijenga miji ya Ono na Lodi, pamoja na vijiji kandokando yake;

13 Beria na Sema walikuwa kati ya jamaa ambazo zilikuwa zinaishi katika muji wa Ayaloni, na kuwafukuza wenyeji wa Gati. Wana wa Beria walikuwa:

14 Ahio, Sasaki, Yeremoti,

15 Zebadia, Aradi, Ederi,

16 Mikaeli, Isipa na Yoa.

17-18 Wana wa Epali walikuwa: Zebadia, Mesulamu, Hezekia, Heberi, Isinerai, Isilia na Yobabu.

19-21 Wana wa Simei walikuwa: Yakimu, Sikiri, Zabudi, Elienai, Siletai, Elieli, Adaya, Beraya na Simuriti.

22-25 Wana wa Sasaki walikuwa: Isipani, Eberi, Elieli, Abudoni, Sikiri, Hanani, Hanania, Elamu, Anetotiya, Ifedeya na Penueli.

26-27 Wana wa Yohamu walikuwa: Samuserai, Seharia, Atalia, Yaresia, Elia na Sikiri.

28 Hao ndio waliokuwa wakubwa wa ukoo zao kulingana na vizazi vyao. Walikuwa wanaishi Yerusalema.

29 Yeieli alikuwa mwanzilishi wa muji wa Gibeoni. Muke wake aliitwa Maka.

30 Muzaliwa wake wa kwanza alikuwa: Abudoni. Wana wake wengine walikuwa: Zuri, Kisi, Bali, Nadabu,

31 Gedori, Ahio, Zekeri,

32 na Mikiloti baba ya Simea. Hawa vilevile waliishi Yerusalema karibu na watu wengine wa ukoo wao.


Ukoo wa mufalme Saulo

33 Neri alizaa Kisi, Kisi alizaa Saulo. Saulo alizaa: Yonatani, Malkisua, Abinadabu na Esibali.

34 Mwana wa Yonatani alikuwa: Meribu-Bali; Meribu-Bali alizaa Mika.

35 Wana wa Mika walikuwa: Pitoni, Meleki, Terea na Ahazi.

36 Ahazi alizaa Yera. Naye Yera alizaa Alemeti, Azimaweti na Zimuri. Zimuri alizaa Moza.

37 Moza alizaa Binea, Binea alizaa Rafa, aliyemuzaa Eleasa, naye Eleasa alizaa Azeli.

38 Wana wa Azeli walikuwa: Azirikamu, Bokeru, Isimaeli, Searia, Obadia na Hanani. Wote hao walikuwa wana wa Azeli.

39 Nao wana wa ndugu yake Eseki walikuwa: Ulamu, muzaliwa wake wa kwanza; Yeusi, wa pili; na Elifeleti wa tatu.

40 Wana wa Ulamu walikuwa watu mashujaa sana wa vita, na wapiga upinde hodari. Alikuwa na wana na wajukuu wengi, jumla yao walikuwa mia moja makumi tano. Hao wote waliotajwa hapo juu walikuwa wa ukoo wa Benjamina.

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
Lean sinn:



Sanasan