1 Mambo ya Siku 7 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002Wazao wa Isakari 1 Isakari alikuwa na wana wane: Tola, Pua, Yasubu na Simuroni. 2 Wana wa Tola walikuwa: Usi, Refaya, Yerieli, Yamai, Ibusamu na Semweli. Hao walikuwa wakubwa wa jamaa za ukoo za Tola na watu mashujaa sana wa vita nyakati zao. Hesabu ya wazao wao siku za utawala wa mufalme Daudi ilikuwa elfu makumi mbili na mbili na mia sita. 3 Mwana wa Usi alikuwa: Isirahia. Wana wa Isirahia walikuwa: Mikaeli, Obadia, Yoeli na Isia. Wote watano walikuwa wakubwa wa jamaa. 4 Kwa vile wake na watoto wao walikuwa wengi sana, walikuwa na wanaume elfu makumi tatu na sita wanaoweza kuenda kwa vita. 5 Ndugu zao katika jamaa zote za kabila la Isakari walioandikwa kwa kufuata ukoo, walikuwa elfu makumi munane na saba, na wote walikuwa mashujaa wa vita. Wazao wa Benjamina na Dani 6 Benjamina alikuwa na wana watatu: Bela, Bekeri na Yediaeli. 7 Bela alikuwa na wana watano: Esiboni, Usi, Usieli, Yeremoti na Iri. Hawa walikuwa viongozi wa jamaa zao, na waaskari mashujaa. Walioandikwa kwa kufuata ukoo na hesabu ya wazao wao ilikuwa elfu makumi mbili na mbili na makumi tatu na wane. 8 Wana wa Bekeri walikuwa: Zemira, Yoasi, Eliezeri, Eliehonai, Omuri, Yeremoti, Abiya, Anatoti na Alemeti. Wote hawa ni wazao wa Bekeri. 9 Waliandikishwa kwa ukoo kulingana na vizazi vyao kama viongozi wa jamaa zao, na hesabu ya wazao wao ilikuwa elfu makumi mbili na mia mbili, wote wakiwa mashujaa wa vita. 10 Mwana wa Yediaeli alikuwa: Bilihani. Wana wa Bilihani walikuwa: Yeusi, Benjamina, Ehudu, Kenana, Zetani, Tarsisi na Ahisahari. 11 Wote hawa walikuwa wakubwa wa jamaa katika ukoo zao na waaskari mashujaa wa vita. Kutokana na wazao wao, kulipatikana wanaume elfu kumi na saba na mia mbili, waaskari hodari tayari kabisa kwa vita. 12 Supimu na Hupimu walikuwa wana wa Iri. Husimu alikuwa mwana wa Aheri. Wazao wa Nafutali 13 Nafutali alikuwa na wana wane: Yazieli, Guni, Yereri na Salumu. Hao walikuwa wazao wa Biliha. Wazao wa Manase 14 Manase alikuwa na wana wawili kutoka kwa habara yake Mwaramu: Asirieli na Makiri. Makiri alikuwa baba ya Gileadi 15 Makiri alizaa Hupimu na Supimu. Jina la dada yake lilikuwa Maka. Mwana wa pili wa Makiri aliitwa Zolofehadi. Zolofehadi alikuwa na wabinti peke yake. 16 Maka muke wa Makiri, alizaa mwana jina lake Peresi. Jina la ndugu ya Peresi lilikuwa Seresi. Wana wa Seresi walikuwa Ulamu na Rakemu. 17 Rakemu alizaa Bedani. Hawa wote ni wazao wa Gileadi, mwana wa Makiri, mujukuu wa Manase. 18 Hamo-Leketi, dada ya Gileadi, alizaa: Isihodi, Abiezeri na Mala. 19 Wana wa Semida walikuwa: Ahiana, Sekemu, Liki na Aniamu. Wazao wa Efuraimu 20-21 Hawa ndio wazao wa Efuraimu: Sutela alizaa Beredi, Beredi alizaa Tahati, Tahati alizaa Eleada, Eleada alizaa Tohati, Tohati alizaa Zabadi, Zabadi alizaa Sutela. Zaidi ya hao, Efuraimu alikuwa na wana wengine wawili, Ezeri, na Eleadi, ambao waliuawa na wenyeji wa asili wa inchi ya Gati kwa sababu walikwenda kule kuwanyanganya ngombe zao. 22 Efuraimu baba yao aliomboleza vifo vyao kwa siku nyingi sana, na wandugu zake wakakuja kumufariji. 23 Halafu Efuraimu akalala na muke wake, naye akapata mimba na kuzaa mwana. Efuraimu akamupa jina la Beria, kwa sababu ya magumu yaliyopata jamaa yake. 24 Efuraimu alikuwa na binti jina lake Sera. Huyu ndiye aliyejenga miji ya Beti- Horoni ya juu na ya chini, na Uzeni-Sera. 25-27 Efuraimu alizaa vilevile Refa, Refa alizaa Resefi, Resefi alizaa Tela, Tela alizaa Tahani, Tahani alizaa Ladani, Ladani alizaa Amihudi, Amihudi alizaa Elisama, Elisama alizaa Nuni, Nuni alizaa Yoshua. 28 Inchi zao na makao yao yalikuwa: Beteli na vijiji vyake, muji wa Narani uliokuwa upande wa mashariki, muji wa Gezeri uliokuwa upande wa magaribi pamoja na vijiji vyake, Sekemu na vijiji vyake, na Aya na vijiji vyake. 29 Na vilevile kwenye mipaka ya wana wa Manase: Beti-Seani na vijiji vyake, Tanaki na vijiji vyake, Megido na vijiji vyake na Dori na vijiji vyake. Hiyo ndiyo miji ambomo wazao wa Yosefu, mwana wa Israeli walimoishi. Wazao wa Aseri 30 Wana wa Aseri walikuwa: Imuna, Isiwa, Isiwi na Beria, pamoja na binti mumoja jina lake Sera. 31 Wana wa Beria walikuwa: Heberi na Malkieli, aliyekuwa baba ya watu wa muji wa Birza-Iti. 32 Wana wa Heberi walikuwa: Yafuleti, Someri na Hotamu, na binti mumoja jina lake Sua. 33 Wana wa Yafuleti walikuwa: Pasaki, Bimuhali na Asiwati. 34 Wana wa Someri walikuwa: Roga, Yehuba, na Aramu. 35 Wana wa Helemu walikuwa: Sofa, Imuna, Selesi na Amali. 36 Wana wa Sofa walikuwa: Sua, Harneferi, Suali, Beri, Imura, 37 Bezeri, Hodi, Sama, Silisa, Itirani na Bera. 38 Wana wa Yeteri walikuwa: Yefune, Pisipa na Ara. 39 Wana wa Ula walikuwa: Ara, Hanieli na Risia. 40 Hao wote walikuwa wazao wa Aseri na walikuwa wakubwa wa jamaa zao, watu wafundi na hodari wa vita. Hesabu ya wale walioandikwa kwa kufuata ukoo katika kundi la waaskari ilikuwa elfu makumi mbili na sita. |
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.
Bible Society of the Democratic Republic of Congo