Biblia Todo Logo
Bìoball air-loidhne

- Sanasan -

1 Mambo ya Siku 10 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002


Kifo cha mufalme Saulo
( 1 Sam 31.1-13 )

1 Siku moja, Wafilistini wakapigana vita na Waisraeli; nao Waisraeli wakakimbia mbele ya Wafilistini na kuuawa katika mulima wa Gilboa.

2 Lakini Wafilistini wakamuzunguka Saulo na wana wake, kisha wakawaua Yonatani, Abinadabu na Malikisua wana wa Saulo.

3 Vita ilikuwa kali sana juu ya Saulo. Wapiga mishale walipomwona wakamwumiza sana.

4 Kwa hiyo Saulo akamwambia mutu aliyemubebea silaha: “Chomoa upanga wako unichome nikufe, kusudi watu hawa wasiotahiriwa wasikuje kunichekelea.” Lakini yule aliyemubebea silaha hakutaka kufanya vile; aliogopa sana. Halafu, Saulo alitwaa upanga wake mwenyewe akauangukia.

5 Wakati yule aliyemubebea silaha alipoona kwamba Saulo amekufa, naye vilevile akauangukia upanga wake, akakufa.

6 Hivi ndivyo Saulo alivyokufa, yeye na wana wake watatu, na jamaa yake yote.

7 Nao watu wa Israeli walioishi katika bonde walipoona waaskari wamekimbia waadui, na kwamba Saulo na wana wake wamekufa, wakahama toka miji yao, wakakimbia. Wafilistini wakaenda na kukaa katika miji hiyo.

8 Kesho yake, Wafilistini walipokwenda kutwaa vitu vya wale waliouawa, wakakuta maiti ya Saulo na wana wake kwenye mulima Gilboa.

9 Wakamvua nguo, wakatwaa kichwa chake pamoja na silaha zake, halafu wakatuma wajumbe katika inchi yote ya Filistia kutangaza habari kwa sanamu zao na watu.

10 Wakaweka silaha za Saulo katika hekalu la miungu yao, kisha wakatundika kichwa chake katika hekalu la Dagoni.

11 Lakini watu wa Yebesi Gileadi waliposikia yote Wafilistini waliyomutendea Saulo,

12 mashujaa wote wakaondoka na kutwaa mwili wa Saulo na miili ya wana wake, wakaileta mpaka Yabesi. Wakazika mifupa yao chini ya muti wa mwalo kule Yabesi, nao wakafunga kula kwa muda wa siku saba.

13 Saulo alikufa kwa sababu ya kutokuwa mwaminifu; hakukuwa mwaminifu maana hakutii neno la Yawe na alikwenda kwa mwaguzi kumwomba shauri,

14 pahali pa kumwendea Yawe kwa kumwomba shauri. Kwa sababu hiyo Yawe akamwua, na akamupa Daudi mwana wa Yese ufalme wake.

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
Lean sinn:



Sanasan