Timiza maagizo ya Yawe, Mungu wako, ufuate njia zake na kushika masharti yake, amri zake, maagizo yake na maamuzi yake kama ilivyoandikwa katika Sheria ya Musa. Kwa hiyo, utafanikiwa katika kila jambo unalofanya na kokote unakoenda.
bila kujitukuza mwenyewe juu ya wandugu zake, wala kuiweka kando amri hii kwa namna yoyote, kusudi aweze kudumu katika utawala, yeye na wazao wake katika Israeli.
Lakini watu wenye woga, wasioamini, wenye machukizo, wauaji, wazinzi, wachawi, wanaoabudu sanamu na wote wanaosema uongo, fungu lao ni katika lile ziwa la moto na ndani ya mawe ya kiberiti yanayowaka moto. Hiki ndicho kifo cha pili.”