Inchi yote ya Misri itakuwa giza kwa sababu ya nzige wale. Watakula kila kitu kilichobaki nyuma ya ile mvua ya mawe. Vilevile hawataacha chochote juu ya miti inayoota katika mashamba.
Nitawaimarisha watu wa Yuda; nitawaokoa wazao wa Yosefu. Nitawarudisha kwao kwa maana ninawaonea huruma, nao watakuwa kama vile sikuwa nimewakataa. Mimi ni Yawe, Mungu wao, nami nitayasikiliza maombi yao.