Nawe Musa umulete kwangu Haruni ndugu yako, pamoja na wana wake: Nadabu, Abihu, Eleazari na Itamari. Utawachagua kati ya Waisraeli, kusudi wanitumikie kama vile makuhani.
Haya ndiyo mambo utakayowafanyia Haruni na wana wake kwa kuwatakasa wapate kunitumikia kama vile makuhani. Utatwaa mwana-ngombe dume na kondoo dume wawili wasiokuwa na kilema,
Utawafunga mikaba katika viuno na kuwavalisha kofia zao. Hivi ndivyo utakavyowatakasa Haruni na wana wake kuwa makuhani. Hao watakuwa makuhani siku zote kwa ajili ya sharti la siku zote.
Utwae Haruni na wana wake na zile nguo takatifu, mafuta ya kupakaa, ngombe wa sadaka kwa ajili ya zambi, kondoo dume wawili, na kitunga cha mikate isiyotiwa chachu.