Walawi 6:3 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
3 Kisha kuhani akiwa amevaa nguo yake ya kitani na kapitula yake ya kitani, atatwaa majivu ya ile sadaka kutoka juu ya mazabahu na kuyaweka kando ya mazabahu.
Watakapotoka kwenda kwenye kiwanja cha inje kwa watu, watatosha nguo walizovaa wakati walipokuwa wanatumika na kuziweka katika vyumba vitakatifu. Ni lazima wavae nguo zingine, kusudi watu wasijitakase kwa kugusa nguo zao.
Ataoga mwili wote katika maji, kisha atavaa nguo takatifu. Ataingia pahali pale akiwa amevaa nguo takatifu: koti la kitani na atavaa kapitula ya kitani na akiwa amevaa kanzu ya kitani na kujifunga mukaba wa kitani.
Yawe wa majeshi anasema kwamba yeye mwenyewe ataipeleka laana hiyo. Itapenya kila nyumba ya mwizi na kila nyumba ya mwenye kuapa uongo kwa kutumia jina lake; itakaa mule na kuteketeza nyumba hiyo yote, mbao na mawe.
Yawe wa majeshi anasema: Kisha nitawakaribia kwa kuwahukumu. Sitasita kutoa ushuhuda juu ya wachawi, wazinzi, watoa ushuhuda wa uongo, wanaopunja mushahara wa watumishi, wanaowatesa wajane na wayatima, wanaozuia mugeni asipate haki yake na wale wasioniogopa mimi.