Walawi 2:16 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
16 Kuhani atateketeza sehemu ya sadaka hiyo ya ngano iliyopondwa na mafuta pamoja na ubani wake wote, ikuwe sadaka ya ukumbusho. Hiyo ni sadaka Yawe anayotolewa kwa moto.
Roho wa Bwana wetu Yawe yuko pamoja nami, maana Yawe amenichagua, akanituma niwahubirie wanaoteswa habari njema, niwatunze waliovunjika moyo, niwatangazie waliohamishwa kwamba watapata uhuru, na wafungwa kwamba watafunguliwa.
Lakini matumbotumbo na miguu ya nyama yule vitasafishwa kwa maji. Kuhani atateketeza sadaka yote juu ya mazabahu. Hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumupendeza Yawe.
Ukimutolea Yawe sadaka ya mazao yako ya kwanza utaitoa hiyo ikiwa imechomwa katika masuke yake, au utaitoa katika mikate ya kuchomwa iliyotengenezwa kwa ngano iliyosagwa.
Kuhani atatwaa sehemu ya sadaka hiyo ikiwa ni sadaka ya ukumbusho na kuiteketeza juu ya mazabahu. Hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumupendeza Yawe.
Wakati Yesu alipoishi katika dunia, aliomba na kusihi kwa malalamiko makubwa pamoja na kutoa machozi kwa Mungu ambaye angeweza kumwokoa toka katika kifo. Mungu alimusikia Yesu kwa sababu yeye alimuheshimu.