Tena Mungu akamwambia: “Mimi ni Mungu Mwenye Nguvu. Ujaliwe wazao wengi na kuongezeka. Taifa na kundi la mataifa watatokea kwako na wafalme watatokea katika uzao wako.
Ukuhani ndio ulikuwa musingi wa Sheria iliyotolewa kwa Waisraeli. Basi ikiwa ukamilifu ulipatikana kwa njia ya kazi ya ukuhani wa uzao wa Lawi, hakungekuwa tena lazima kutokee kuhani mwingine anayekuwa sawa na Melkisedeki, kwa pahali pa kuhani anayekuwa sawa na Haruni.
Wazao wa Lawi wanaopewa kazi ya ukuhani wanaamriwa na Sheria kukongoa fungu moja la kumi la mapato toka kwa wandugu zao Waisraeli, ijapokuwa wao vilevile ni wa uzao wa Abrahamu.