Ukuhani ndio ulikuwa musingi wa Sheria iliyotolewa kwa Waisraeli. Basi ikiwa ukamilifu ulipatikana kwa njia ya kazi ya ukuhani wa uzao wa Lawi, hakungekuwa tena lazima kutokee kuhani mwingine anayekuwa sawa na Melkisedeki, kwa pahali pa kuhani anayekuwa sawa na Haruni.
Hakuna mambo yaliyoandikwa juu ya baba ya Melkisedeki, wala mama yake, wala majina ya babu zake. Tena, habari za kuzaliwa kwake na za kufa kwake hazijulikani. Anafanana na Mwana wa Mungu kwa kuwa yeye ni kuhani kwa milele.