Biblia Todo Logo
Διαδικτυακή Βίβλος

- Διαφημίσεις -




Waebrania 11:4 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

4 Kwa njia ya imani, Abeli alimutolea Mungu sadaka nzuri zaidi kuliko ile ya Kaina. Kwa ajili ya imani yake alihesabiwa na Mungu kuwa mwenye haki, kwa maana Mungu mwenyewe alikubali sadaka zake. Na kwa imani ile, ingawa Abeli amekwisha kufa, angali anasema.

Δείτε το κεφάλαιο αντίγραφο




Waebrania 11:4
21 Σταυροειδείς Αναφορές  

Yawe akasema: “Umefanya nini? Damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika udongo.


Lakini Yawe akamujibu: “Hapana, sivyo! Atakayekuua wewe Kaina atalipizwa mara saba.” Basi, Yawe akamutia Kaina kitambulisho hata yeyote atakayemwona asimwue.


Adamu akalala tena na Eva muke wake, naye akazaa mutoto mwanaume, akamwita Seti akisema: “Mungu amenijalia mutoto pahali pa Abeli aliyeuawa na Kaina.”


Kisha Kaina akasemezana na ndugu yake Abeli. Basi, walipokuwa katika shamba, Kaina akamushambulia ndugu yake Abeli, akamwua.


Mara moja, Yawe akashusha moto, ukaiteketeza sadaka ile ya kuteketezwa, kuni, mawe na mavumbi, na kuyakausha maji yote katika mufereji.


Lakini wao watakufundisha na kukuambia mambo waliyopata kuyatoa katika maarifa yao.


Sadaka ya waovu ni chukizo kwa Yawe, lakini maombi ya watu wa usawa yanamufurahisha Mungu.


Sadaka ya mwovu ni kitu cha kuchukiza sana. Inachukiza zaidi akiitoa kwa nia mbaya.


Yawe akawasha moto ukaiteketeza sadaka ya kuteketezwa na mafuta yaliyokuwa juu ya mazabahu. Watu wote walipoona huo moto wakapiga vigelegele na kuinama uso mpaka chini.


Na hivi mutabeba lazima ya damu iliyomwangwa katika dunia pasipo kosa, tangia kuuawa kwa Abeli aliyekuwa mukamilifu mpaka kuuawa kwa Zakaria, mwana wa Barakia, muliyemwuia kwenye hekalu katikati ya Pahali Patakatifu na mazabahu.


tangia kuuawa kwa Abeli mpaka kuuawa kwa Zakaria kwenye hekalu katikati ya mazabahu na Pahali Patakatifu. Kweli ninawaambia: watu wa kizazi hiki watabeba lazima ya mambo hayo yote.


Wanajidai kwamba wanamujua Mungu, lakini wanamukana kwa matendo yao. Wao ni wenye machukizo, waasi hata hawafai kwa kufanya kazi yo yote nzuri.


Ni kwa sababu ya imani yao babu zetu wameshuhudiwa vizuri na Mungu.


Nasi vilevile tunazungukwa na kundi kubwa kama lile la wale walioshuhudia imani yao. Basi tutupilie mbali vitu vyote vinavyotusonga, nazo zambi zinazotufunga upesi na tukimbie kwa juhudi sana katika mashindano tunayowekewa.


Mumefikia karibu na Yesu anayekuwa mupatanishi wa agano jipya, na kwenye damu yake iliyomwangwa inayosema nasi maneno mema zaidi kuliko damu ya Abeli.


Kila Kuhani Mukubwa aliyechaguliwa kati ya watu amesimikwa kwa kumutumikia Mungu kwa ajili ya watu kusudi atolee matoleo na sadaka kwa ajili ya zambi.


Na kufuatana na Sheria, karibu vitu vyote vinatakaswa kwa damu, nazo zambi haziwezi kusamehewa pasipo kumwangwa kwa damu.


Kwa maana mutu yule mwenye haki aliishi kati ya watu wabaya, akiona na kusikia kila siku mambo yaliyochukiza roho yake ya haki.


Ole kwao! Maana wamefuata njia ya Kaina. Kwa ajili ya kupata mali wameanguka katika kosa Balama alilofanya. Wameangamia kwa sababu wameasi kama vile Kora alivyoasi.


Ακολουθησε μας:

Διαφημίσεις


Διαφημίσεις