Biblia Todo Logo
Διαδικτυακή Βίβλος

- Διαφημίσεις -




Nehemia 13:31 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

31 Nikaagiza matoleo ya kuni kufanyika katika wakati unaopaswa na malimbuko wakati wake. Ee Mungu wangu, unikumbuke kwa ajili ya haya yote na unijalie mema.

Δείτε το κεφάλαιο αντίγραφο




Nehemia 13:31
10 Σταυροειδείς Αναφορές  

kwa ajili ya mikate mitakatifu, sadaka za unga za kawaida, sadaka za kuteketezwa kwa moto za kawaida, sadaka za siku za Sabato, sikukuu za mwandamo wa mwezi, sikukuu nyingine zilizowekwa, vitu vingine vitakatifu, sadaka za kusamehewa zambi, kwa kuwafanyia upatanisho watu wa Israeli na kazi nyingine zozote za nyumba ya Mungu wetu.


Sisi wote, watu wote, makuhani na Walawi tutapiga kura kila mwaka kwa kuchagua ukoo utakaoleta kuni za kuteketeza sadaka juu ya mazabahu ya Yawe, Mungu wetu, kufuatana na Sheria.


Kila unga wetu wa kwanza, matoleo yetu, matunda ya miti, divai na mafuta tutavileta kwa kuhani kwenye vyumba vya nyumba ya Mungu wetu. Tena tutaleta zaka zetu za mazao yetu kwa Walawi, maana ndio wanaoshugulika na kukusanya zaka zile katika vijiji vyetu.


Ee Mungu wangu, unikumbuke kwa ajili ya haya yote na usiyasahau matendo yangu mema niliyofanya kwa ajili ya nyumba yako na kwa ajili ya kazi yako.


Nikaagiza Walawi kujitakasa na kwenda kulinda milango kwa kutakasa siku ya Sabato. Ee, Mungu wangu, unikumbuke hata na kwa hili vilevile unihurumie kutokana na rehema zako kubwa.


Sasa, Ee Mungu wangu, kumbuka wema wangu wote niliowatendea watu hawa.


Unikumbuke, ee Yawe, unapowaonyesha watu wako upendo. Unisaidie wakati unapowaokoa,


Usikumbuke zambi na makosa ya ujana wangu; unikumbuke kwa kadiri ya wema wako, kwa ajili ya uzuri wako, ee Yawe.


Na akaongeza kusema: “Ee Yesu, usinisahau wakati utakapokuja katika ufalme wako!”


Ακολουθησε μας:

Διαφημίσεις


Διαφημίσεις