Halafu Mungu akafanya agano na Abrahamu, na kitambulisho cha kuhakikisha kwamba limeshikwa kilikuwa kutahiriwa. Kwa hiyo Abrahamu akamutahiri mwana wake Isaka alipotimiza siku nane za kuzaliwa. Naye Isaka akamutahiri mwana wake Yakobo, na Yakobo akawatahiri wana wake kumi na wawili waliokuwa babu zetu wakubwa.