Kama vile mimi Yawe nilivyoiangamiza miji ya Sodoma na Gomora na miji ya jirani, vilevile hakutakuwa mutu yeyote atakayeishi humo. Kweli, hakuna mutu yeyote atakeyekaa huko. –Ni ujumbe wa Yawe.
Yesu akaingia ndani ya hekalu, naye akawafukuza watu wote waliokuwa wakiuzishia na kununulia vitu vyao ndani yake. Akapindua meza za wale waliobadilisha feza na viti vya wachuuzi wa njiwa.
Siku zile watu walikuwa wakikula na kunywa, wakioa na kuolewa mpaka ilipotimia siku ile Noa alipoingia ndani ya chombo. Halafu mvua kubwa ikanyesha na kuwaangamiza wote.