Wazao wako watakuwa wengi kama mavumbi ya dunia, na urizi wao utaenea kila pahali: upande wa magaribi, mashariki, kaskazini na kusini. Kwa njia yako na ya wazao wako, jamaa zote katika dunia zitabarikiwa.
Nilipopita tena karibu nawe, nikakuona. Wakati huu, ulikuwa umefikia umri wa kupendwa kama binti. Nikalitandaza vazi langu juu yako na kuufunika uchi wako. Nikafanya nawe agano la ndoa, nawe ukakuwa wangu. –Ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe.
Wayuda wamegeuka waadui za Mungu kwa sababu ya kukataa Habari Njema, na jambo hilo limekuwa faida kwenu ninyi watu wa mataifa mengine. Lakini wao ni wapendwa wake kufuatana na vile wamechaguliwa naye, kwa njia ya babu zao.
ndilo taifa la Waisraeli. Wao walikubaliwa na Mungu kuwa watoto wake, yeye aliwaonyesha utukufu, alifanya maagano nao, aliwapa Sheria, aliwaonyesha namna ya kumwabudu na kuwatolea ahadi zake.