Watu wote wanaotengeneza sanamu za miungu ni bure kabisa; na vitu hivyo wanavyovifurahia haviwafalii kitu chochote. Wanaoshuhudia hiyo miungu ya uongo ni vipofu na wajinga. Kwa hiyo hao watafezeheshwa!
Yawe anasema: Piga kelele, wala usijizuize; ulalamike kwa sauti kubwa kama baragumu. Uwatangazie watu wangu makosa yao, uwaambie wazao wa Yakobo zambi zao.
Nitawalipiza maovu yao wayalipe vilevile maovu ya babu zao. –Ni Yawe anayesema hivyo.– Wao waliifukizia ubani miungu yao kwenye milima, wakanitukana mimi kule juu ya vilima. Nitawalipa sawa inavyostahili, watayalipa matendo yao ya zamani.
“Ole kwenu, ninyi walimu wa Sheria na Wafarisayo, ninyi wanafiki! Munawafungia watu wengine njia ya kuingia katika Ufalme wa mbinguni. Ninyi wenyewe hamwingii mule na zaidi ya hii munawazuiza wale wanaotaka kuingia. [
Wanafanya matendo yao yote tu kusudi wajionyeshe mbele ya watu. Wanajifungia kwa paji za nyuso vibweta vipana vyenye vikaratasi vya Maandiko Matakatifu. Nao wanavaa kanzu zenye pembe ndefu.