Biblia Todo Logo
Διαδικτυακή Βίβλος

- Διαφημίσεις -




Isaya 16:8 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

8 Mashamba ya Hesiboni yamefifia, vilevile na zabibu za Sibuma ambazo ziliwalewesha wakubwa wa mataifa. Zikafika Yaweri na kusambaa hata katika jangwa, chipukizi zake zikafika hata ngambo ya bahari.

Δείτε το κεφάλαιο αντίγραφο




Isaya 16:8
13 Σταυροειδείς Αναφορές  

Enyi milima ya Gilboa, musikuwe na umande au mvua juu yenu. Wala mashamba yenu yasitoe chochote siku zote. Maana kule ngao za shujaa zilichafuliwa, ngao ya Saulo haikupakaliwa mafuta.


Lakini Asuria hakuwazia hivyo, yeye alikuwa na nia ingine; alikusudia kuharibu kabisa, kuangamiza mataifa mengi sana.


Watu wa Hesiboni na Eleale wanalia, sauti zao zinasikilika mpaka Yasa. Hata waaskari wa Moabu wanalia kwa sauti; mioyo yao inatetemeka.


Kwa hiyo ninalia pamoja na Yaweri kwa ajili ya mizabibu ya Sibuma. Machozi yananitoka kwa ajili yenu, enyi miji ya Hesiboni na Eleale; maana vigelegele vya mavuno ya matunda na ya ngano vimetoweka.


Mizabibu inanyauka, divai inakosekana. Wote waliokuwa wenye furaha sasa wanaugua kwa huzuni.


Ninakulilia wewe muzabibu wa Sibuma kuliko hata watu wa Yazeri. Matawi yako yametanda mpaka ngambo ya bahari ya Chumvi, yakafika hata mpaka Yazeri. Lakini mwangamizaji ameyarukia matunda yako ya wakati wa jua na mizabibu yako.


Kisha Musa akatuma watu wapeleleze muji wa Yazeri; wakauteka pamoja na vijiji vyake, wakawafukuza Waamori waliokaa humo.


Miji ya Ataroti, Diboni, Yazeri, Nimura, Hesiboni, Eleale, Sebamu, Nebo na Beoni,


Aturoti-Sofani, Yazeri, Yogibeha,


Nebo na Bali-Meoni (majina ya hiyo miji yalibadilishwa), na Sibuma. Miji waliyoijenga wakaipa majina mengine.


Kiriataimu, Sibuma, Zereti-Sahari, kule kwa kilima katika bonde,


ilikuwa Yazeri, miji yote ya Gileadi na nusu ya inchi ya Waamoni mpaka Aroeri kwa upande wa mashariki wa Raba.


Ακολουθησε μας:

Διαφημίσεις


Διαφημίσεις