Utatengeneza kinara cha taa kwa zahabu safi. Tako lake na muti wa kile kinara vitakuwa kitu kimoja, vilevile na vikombe vyake. Mafundo yake na maua yake, vyote vitafuliwa kwa kipande kimoja tu cha zahabu.
Halafu watatandaza kitambaa cha rangi ya samawi juu ya mazabahu ya zahabu na kuifunika kwa ngozi laini ya mbuzi. Halafu wataingiza miti yake ya kuibebea.
Watatwaa vyombo vyote vinavyotumika katika Pahali Patakatifu, watavifunga kwa kitambaa cha rangi ya samawi na kuvifunika kwa ngozi laini ya mbuzi, kisha wataviweka juu ya miti yake ya kubebea.
Juu yake wataweka kifuniko cha ngozi laini ya mbuzi, kisha watatandaza juu yake kitambaa cha rangi ya samawi tupu. Halafu wataingiza miti ya kulibebea sanduku hilo.
Watatwaa kitambaa cha rangi ya samawi ambacho watafunikia kinara cha taa na taa zake, makasi zake, sinia zake na vyombo vyote vinavyotumiwa kukiwekea mafuta.