Muingie katika mapango chini ya mawe, katika mashimo ndani ya udongo, kwa kuepuka kitisho cha Yawe, mbali na mwangaza wa utukufu wake, atakapokuja kuogopesha dunia.
Nao wataingia katika mapango chini ya mawe na kwenye nyufa za mawe, kwa kuepuka kitisho cha Yawe, mbali na mwangaza wa utukufu wake, atakapokuja kuogopesha dunia.
Hata wakijificha juu ya mulima Karmeli, huko nitawatafuta na kuwakamata; hata wakijificha mbali nami katika vilindi vya bahari, mule nitaiamuru nyoka kubwa ya bahari iwaume.
Watatambaa katika mavumbi kama nyoka, kama viumbe vinavyotambaa. Watatoka katika makimbilio yao wakitetemeka na kujaa hofu. Watakugeukia Yawe, Mungu wetu, kwa hofu, wataogopa kwa sababu yako.
Jua linatokea na kwa joto kali linakausha mimea, nayo maua yake yanaanguka na uzuri wake wote unaharibika. Hivi ndivyo tajiri naye atakavyotoweka katika shuguli zake.