Nitamwambia Yawe kwa moyo wangu wote: “Wewe, ee Yawe, hakuna anayekuwa kama wewe! Wewe unawaokoa wamasikini kutoka makucha ya wenye nguvu, wamasikini na wakosefu kutoka mikono ya wanyanganyi.”
Lakini Bwana alinisaidia, akanitia nguvu nipate kuitangaza Habari Njema kwa ukamilifu kusudi watu wa mataifa mengine wapate kuisikia. Nami nikaokolewa toka katika kinywa cha simba.