Hapo roho wa Yawe akamushika Samusoni kwa nguvu, naye akaenda muji Askeloni, akawaua watu makumi tatu, kisha akatwaa nguo zao za sikukuu, akawapa wale waliotegua kitendawili chake. Halafu akaondoka, akaenda kwa nyumba kwa wazazi wake akiwa na hasira kali.